29 May 2010

CONSOLATA LUKOSI ATWAA TAJI LA MISS TABATA 2010

Miss Tabata 2010 CONSOLATA LUKOSI akipunga mkono kwa furaha
Washindi wa Tano bora wakiwa na mshindi wa miss Tabata CONSOLATA LUKOSI katikati
Presha inapanda presha inashuka............Conso na Cythia walipokuwa wanasubiri kusikia nani kati yao atatwaa taji la miss Tabata 2010
Mrembo wa mwaka jana Everlyne Gamassa akimvisha skafu ya ushindi Conso

Miss Tabata 2010 CONSOLATA LUKOSI akipungia mkono mashabiki mara baada ya kutangazwa mshindi katika shindano lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa D`a West Park Tabata jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo kulia ni mshindi wa tatu Lilian Andrew na kushoto ni mshindi wa pili Cynthia Bavo.

28 May 2010

MISS TABATA LEO, KUZOA 500,000/-

Mashindano ya kumtafuta mrembo wa Tabata, Miss Tabata 2010, litafanyika leo katika ukumbi wa Dar West Park ambapo mshindi wake atazawadiwa jumla ya shilingi 500,000.

Mratibu wa shindano hilo, Godfrey Kalinga, alisema jana walipokutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa Savanna Lounge kuwa mshindi wa pili atajinyakulia shilingi 350,000 na mshindi wa tatu atazawadiwa shilingi 250,000.

Warembo wengine watakaoingia tano bora watazawadiwa shilingi 150,000 kila mmoja na wengine watakaofanikiwa kuingia katika hatua ya 10 bora kila mmoja atapewa shilingi 100,000.

Warembo waliyosalia watapewa kifutajasho cha shilingi 50,000 kila mmoja. Mbali na zawadi waremo zaidi ya kumi watafuzu kushiriki kwenye mashindano ya kanda ya Ilala, Miss Ilala 2010.

Washiriki wa Miss Tabata ni Ritha Swai (19), Upendo Paul (18), Jesca Mariwa (19), Ummy Mohamed (22), Benardina Mwita (18), Maria Mpete (22) na Cythia Baro (22). Wengine ni Happyness Paul (21), Happy Mushi (20), Neema Chaky (18), Consolata Lukosi (20), Rose Anthony (23), Light Mziray (20), Bellynda Mselewa (20), Harrieth Mulumba (20), Lilian Andrew (19), Selina Wangusu (21) na Doreen Deus (18).

Warembo hao wamekuwa wakifundishwa na Rehema Uzuia, Stella Solomon and Abdilahi Zungu.

Bendi ya African Stars “Wazee wa Kisigino” watatumbuiza kwenye shindano hilo ambalo limedhaminiwa na Vodacom, Overmeer Wine, East Africa Radio, EATV, Chicken Hut, Savanna Lounge, PSI, Fabak Fashion, Dreditto Entertainment, Screen Masters, Benchmark Productions na USA-Dars General Supplies.

Everlyne Gamasa ndiye anayeshikilia taji la Miss Tabata kwa sasa. Miss Tabata namba mbili wa mwaka jana Julieth William ndiye Vodacom Miss Tanzania namba tatu kwa sasa.

Miss Tabata imeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.

24 May 2010

KAMATI YA MISS TANZANIA ILIPOTEMBELEA KAMBI YA MISS TABATA 2010



Washiriki wa miss Tabata 2010 wakipozi kwa picha katika ukumbi wa Da` West Tabata kabla ya kufika kamati ya miss Tanzania ilioongozwa na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga
........................................................................................................................................................................


Lundenga awavulia kofia Miss Tabata

Mkurugenzi wa Miss Tanzania Hashim Lundenga juzi alivutiwa na maandalizi ya warembo wanaoshiriki kwenye shindano la Miss Tabata ambao limepangwa kufanyika Ijumaa katika Ukumbi wa Dar West Park , Tabata.

Lundenga alisema wengi wa warembo hao wanasifa ya kushinda taji la Vodacom Miss Tanzania iwapo watajiamini na kutofuata tabia mbaya zinazofanywa na baadhi ya warembo waliyowahi kushiriki kwenye mashindano hayo.

Lundenga alisema hayo wakati alipotembelea kambi ya warembo wanaoshiriki Miss Tabata Jumapili katika ukumbi wa Dar West Park ambapo alisema kamati yake ni safi lakini tabia chafu zinazofanywa na baadhi ya warembo waliyowahi kushinda mataji mbali mbali zinafanya kamati yake ionekane haifai.

“Sisi tunaka na nyinyi siku 30 tu ambazo ni chache mno kutufanya tujue tabia zenu. Warembo wengi huwa wanaficha tabia zao wanaposhiriki lakini baada ya kushinda huwa huonyesha tabia zao mbaya kwa jamii,” Lundenga aliwaambia warembo hao.

“Tumegundua kuwa warembo wengi huwa nanapakaziwa na huonewa lakini hawana tabia mbaya,” mkurugenzi huyo alisema.

Warembo watakaoshiriki kwenye shindano la Miss Tabata ambalo litafanyika Ijumaa katika ukumbi wa Dar West, Tabata ni Ritha Swai (19), Upendo Paul (18), Jesca Mariwa (19), Ummy Mohamed (22), Benardina Mwita (18), Maria Mpete (22) na Cythia Baro (22).

Wengine ni Happyness Paul (21), Happy Mushi (20), Neema Chaky (18), Consolata Lukosi (20), Rose Anthony (23), Light Mziray (20), Bellynda Mselewa (20), Harrieth Mulumba (20), Lilian Andrew (19), Selina Wangusu (21) na Doreen Deus (18).

Warembo hao watakutana na majaji kesho kwenye prejudgement. Zawadi za washindi zitatangazwa Alhamisi kwenye kikao cha pamoja na waandishi wa habari itakayofanyika kwenye ukumbi wa Savanna Lounge kwenye jengo la Benjamin Mkapa Towers .

Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” watatumbuiza kwenye shindano hilo ambalo taji lake linashikiliwa na Everlyne Gamasa.

Miss Tabata imedhaminiwa na Vodacom, Overmeer Wine, East Africa Radio, EATV, Chicken Hut, Savanna Lounge, PSI, Fabak Fashion, Dreditto Entertainment, Screen Masters, Benchmark Productions, USA-Dars General Supplies.

Warembo zaidi ya 10 watafuzu kushiriki kwenye mashindano ya kanda ya Ilala na baadaye Vodacom Miss Tanzania.

Shindano la Tabata ni moja ya vituo viwili vilivyobakizwa kwenye kanda ya Ilala baada ya vingine vitatu kufutwa na waandaaji wa taifa.

Miss Tabata namba mbili wa mwaka jana Julieth William ndiye Vodacom Miss Tanzania namba tatu kwa sasa.
Mwenyekiti wa Miss Tabata Fred Ogot (katikati) akiwa na mratibu wa miss Tabata Mr GOD (kushoto) wakijadili jambo kabla ya kuwasili kwa Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga
Mrembo Light Mziray na Ritha Swai
Miss Tabata mwaka 2009 Everlyne Gamassa akiongea na washiriki wa miss Tabata 2010
Washiriki wa miss Tabata 2010 wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga
Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga
Warembo wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania
Miss Tabata mwaka 2009 Everlyne Gamassa
Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga akisisitiza jambo kwa washiriki wa miss Tabata 2010 alipokuwa akiongea nao katika ukumbi wa Da` West
Mrembo Neema Chaky akimuuliza swali Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga alipowatembelea kambini kwa ukumbi wa Da ` West Tabata
Mrembo Upendo Paul akimuuliza swali Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga alipowatembelea kambini kwa ukumbi wa Da ` West Tabata
Benardina Mwita naye pia alipata fursa ya kuuliza swali kamti ya miss Tanzania
Harrieth Mulumba akiuliza swali kwa kamati ya miss Tanzania


Warembo wa miss Tabata 2010 wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga
Miss Tabata mwaka 2009 Everlyne Gamassa
Baadhi wa washiriki wa miss Tabata 2010
Mwenyekiti wa Miss Tabata Fred Ogot

Walimu wa washiriki wa miss Tabata 2010, Sweet Ney (kulia) na Stella
Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga akisisitiza jambo kwa washiriki wa miss Tabata 2010
Mwenyekiti wa Miss Tabata Fred Ogot akiongea na warembo wake katika ukumbi wa Da' West Tabata.
Miss Tabata mwaka 2009 Everlyne Gamassa( kulia) Sweet Ney pamoja na Stella

Mwenyekiti wa Miss Ilala Mr. Kalikumtima akiongea na warembo wa miss Tabata 2010



Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga (kushoto) akiongea na warembo
''Mkifanya mambo ya utovu wa nidhamu sisi ndio tunalaumiwa ....nawaomba sana mjiheshimu katika kila jambo ili msiichafue sifa ya kamati ya miss Tanzania kwani ina miiko yake na kanuni zinazo iendesha....."
Warembo wa miss Tabata wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa viongozi wa kamati ya miss Tabata iliyowatembelea Jana jioni katika ukumbi wa Da' West Tabata.



20 May 2010

WASHIRIKI MISS TABATA 2010

Washiriki wa kinyang`anyiro cha miss Tabata 2010 wakipozi kwa picha ya pamoja katika ukumbi wanaofanyia mazoezi wa Da' West Park Tabata.
Visura wa miss Tabata 2010 katika pozi la nguvu, si mchezo mwaka huu....

Warembo wakiwa katika mazoezi