Mashindano ya kumtafuta mrembo wa Tabata, Miss Tabata 2010, litafanyika leo katika ukumbi wa Dar West Park ambapo mshindi wake atazawadiwa jumla ya shilingi 500,000.
Mratibu wa shindano hilo, Godfrey Kalinga, alisema jana walipokutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa Savanna Lounge kuwa mshindi wa pili atajinyakulia shilingi 350,000 na mshindi wa tatu atazawadiwa shilingi 250,000.
Warembo wengine watakaoingia tano bora watazawadiwa shilingi 150,000 kila mmoja na wengine watakaofanikiwa kuingia katika hatua ya 10 bora kila mmoja atapewa shilingi 100,000.
Warembo waliyosalia watapewa kifutajasho cha shilingi 50,000 kila mmoja. Mbali na zawadi waremo zaidi ya kumi watafuzu kushiriki kwenye mashindano ya kanda ya Ilala, Miss Ilala 2010.
Washiriki wa Miss Tabata ni Ritha Swai (19), Upendo Paul (18), Jesca Mariwa (19), Ummy Mohamed (22), Benardina Mwita (18), Maria Mpete (22) na Cythia Baro (22). Wengine ni Happyness Paul (21), Happy Mushi (20), Neema Chaky (18), Consolata Lukosi (20), Rose Anthony (23), Light Mziray (20), Bellynda Mselewa (20), Harrieth Mulumba (20), Lilian Andrew (19), Selina Wangusu (21) na Doreen Deus (18).
Warembo hao wamekuwa wakifundishwa na Rehema Uzuia, Stella Solomon and Abdilahi Zungu.
Bendi ya African Stars “Wazee wa Kisigino” watatumbuiza kwenye shindano hilo ambalo limedhaminiwa na Vodacom, Overmeer Wine, East Africa Radio, EATV, Chicken Hut, Savanna Lounge, PSI, Fabak Fashion, Dreditto Entertainment, Screen Masters, Benchmark Productions na USA-Dars General Supplies.
Everlyne Gamasa ndiye anayeshikilia taji la Miss Tabata kwa sasa. Miss Tabata namba mbili wa mwaka jana Julieth William ndiye Vodacom Miss Tanzania namba tatu kwa sasa.
Miss Tabata imeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.