01 June 2011

Miss Tabata watembelea mbuga za Mikumi


Warembo 22 watakaoshiriki kwenye kinyang’anyiro cha kumsaka Miss Tabata 2011 jana waliondoka Dar es Salaam kwenda kutembelea mbuga za wanyama za Mikumi.

Mratibu wa shindano hilo, Joseph Kapinga, alisema jana kuwa lengo la ziara hiyo ni kukuza utalii wa ndani.

“Lengo la ziara hii ni kutangaza utalii wa ndani. Tunataka warembo wetu wajue wanyama na vivutio vingine vinavyopatikana kwenye mbuga zetu hasa Mikumi,” Kapinga alisema.

Alisema kuwa wakiwa Mikumi, warembo hao wapata fursa ya kuwajua tabia za wanyama na ndege wote waliomo kwenye mbuga hiyo.

Miss Tabata imepangwa kufanyika Juni 10 katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.

Warembo walioondoka ni Marion Augustino (19), Neema Marwa (18), Catherine Julius (20), Lilian William (20), Godliver Mashamba (22) na Dorice Mutabingwa (21).

Wengine ni Sweetlily Suleiman (21), Maria John (21), Happyness Emmanuel (18), Cresensia Haule (20), Mariam Manyanya (21), Agustina Mshanga (20), Nasra Salim (21), Faiza Ally (19) na Edina Mnada (21).

Wamo pia Angela Fortunatus (21), Lucia Joseph (20), Lilian Brayson (22), Rita Mvungi (21) na Willieth Wilson (22).

Miss Tabata 2011 inadhaminiwa na Dodoma Wine, Vodacom, Redds Original, Integrated Communications, Paris Pub, Fabak Fashion, Freditto Entertainment, Chicken Hut, Travel Partners, Ben Expedition, Screen Masters, Sean Entertainment, Michuzi blogspot na Anech Stationary.

Consolata Lukosi ndiye mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata 2010.

Mrembo huyo alikuwa nambari tatu mwaka jana kwenye shindano la taifa (Miss Tanzania) kabla ya kushinda taji la Redds Ambassador.

Mashindano hayo ya urembo yanaandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.