02 June 2013

NI DORIS MOLLEL REDD'S MISS TABATA 2013









Redd`s Miss Tabata 2013, Doris Molel akipunga mkono kwa mashabiki wake muda mfupi baada ya kutawazwa rasmi kuwa Mrembo wa Kitongoji cha Tabata, Shindano hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa Da` West Park Jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Mshindi wa Pili wa shindano hilo Upendo Lema (kulia) pamoja na Mshindi wa tatu, Rachel Mushi.


Redd`s Miss Tabata aliyemaliza muda wake Noella Michael (aliyekaa katikati) akisubiri kwa hamu kubwa kutangazwa mrithi wake

Tano bora Miss Tabata 2013

Kumi bora wakijipanga kwa mchujo wa Tano Bora

Kama The Jacko

Kazi imeuma mrembo wa miss Tabata 2013  akilisakata yenu jukwaani

Warembo waliohudhuria Miss Tabata 2013 wakishangilia

Majaji wa Miss Tabata wakiwa kazini kuchmabua pointi

Viongozi wa Miss Tanzania wakimsikiliza Hoyce Temu aliyewahi kuwa Miss Tanzania



Wapenzi wa mambo ya Warembo wakifuatilia kwa mwakini kinachoendelea jukwaani

30 May 2013

WAREMBO WA MISS TABATA 2013 WATEMBELEA THE GUARDIAN

Warembo wa Miss Tabata 2013walipotembelea Kampuni ya The Guardian iliyopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam

15 June 2012

NI KWENYE SHINDANO LA MISS TABATA 2012


Hapa ni watu mbalimbali wali ingia ndani ya nyumba...pia King Kif nilizama sambamba na Said Mdoe kutoka Screen Masters

Costa Siboka kutoka Ukerewe naye kapiga picha na washindi....

Huyu dada ni Lilian Internet kutoka Mashujaa Bend

02 June 2012

NOELA MICHAEL AVIKWA TAJI LA MISS TABATA 2012

Redds Miss Tabata Noela Michael (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wenzake wa hatua ya tatu bora. Kulia ni mshindi wa tatu na kushoto ni Mshindi wa pili Susan Deodatus. Shindano hilo lilishirikisha warembo 18.
Redds Miss Tabata Noela Michael (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wenzake wa hatua ya tano bora na ambao wote wamefanikiwa kupata tiketi ya kuingia katika shindano la Kanda ya Ilala, Miss Ilala 2012. Kushoto ni mshindi wa tano Filos Lemy, Mshindi wa pili Susan Deodatus, Miss Tabata, Mshindi wa tatu na mshindi wan ne, Willemina Mvungi.
Redds Miss Tabata 2012, Noela Michael akipunga mkono kwa furaha baada ya kuvikwa taji hilo usiku wa kuamkia leo kwa kuwashinda warembo wengine 17 waliokuwa wakiwania pamoja taji hilo. Miss Tabata 2012 ilifanyika katika Ukumbi wa Dar West Park Tabata jijini Dar

MAMBOYALIVYOKUWAUSIKUWAKUMSAKAMALKIAWA TABATA




















01 June 2012

MISS TABATA KUFANYIKA LEO, MASHAUZI NA MASHUJAA NDANI YA NYUMBA




Shindano la kusaka Miss Tabata 2012 linafanyika leo (Ijumaa) katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga alisema jana kuwa bendi za Mashauzi Classic na Mashujaa zitawasindikiza warembo 19 watakaopanda jukwaani kuwania taji hilo.
Mratibu wa shindano hilo lililoandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts alisema kuwa mshindi wa kwanza atazawadiwa Sh 500,000/- na king’amuzi ambayo imelipia miezi sita yenye thamani ya sh 800,000 iliyotolewa na Multichoice.
Mshindi wa pili atapata sh 500,000, mshindi wa tatu sh 350,000 wakati washindi wa nne na watano kila moja atapata sh 200,000.
Kapinga alisema warembo watano watawakilisha Tabata kwenye shindano la Miss Ilala.
Warembo wengine watakaoingia 10 bora kila moja atapata sh 100,000 wakati waliyosalia watapata Sh 50,000 kila moja.
Kapinga alisema shindano hilo pia litatumika kwa ajili ya kusherehekea miaka 10 tangu kuasisiwa kwa shindano la Miss Tabata.
“Shindano la mwaka huu sio la kukosa kwani litakuwa ni la aina yake ukizingatia kuwa litatumika kusherekea miaka 10 tangua kuanza kuandaa Miss Tabata,” alisema Kapinga.
Alisema warembo waliyowahi kushinda mataji mbalimbali ya shindano hilo, pia wamealikwa kusherehekea miaka 10 ya Miss Tabata.
Shindano hili limedhaminiwa na Dodoma Wine, Redds, Integrated Communications, Fredito Entertainment, Multichoice Tanzania, Screen Masters, Kitwe General Traders, Step In Electronics, Brake Point, Atriums Hotel na Lady Pepeta.
Mrembo anayeshikilia taji la Tabata kwa sasa ni Faiza Ally.
Warembo wa Tabata wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano ya Miss Tanzania ambapo mwaka juzi Consolata Lukosi alishinda nafasi ya tatu kabla ya kutangazwa kuwa balozi wa kinywaji cha Redds.
Katika shindano la mwaka juzi Juliet William pia alishinda nafasi ya tatu katika ngazi hiyo ya taifa.
Juliet ndiye anayeshikilia taji la dunia la Miss Progressive International.